Ingia / Jisajili

Baba Padre Tunakuaga

Mtunzi: Thomas Andrea Malinga
> Mfahamu Zaidi Thomas Andrea Malinga
> Tazama Nyimbo nyingine za Thomas Andrea Malinga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito | Shukrani

Umepakiwa na: Thomas Malinga

Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Baba Padre tunakuaga, tunakutakia utume mwema uendako x2

Tunakushukuru kwa utume uliotukuka x2 . Tunakupongeza kwa kuteuliwa kuwa Paroko wa Parokia mpya uendako x2.

Hongera Baba Padre kwa utume, Twakutakia utume mwema sana, Mungu awe pamoja na wewe.

MASHAIRI

1. (a) Miaka minne hapa kwetu, hakika ulitulea

    (b) Watoto kutubatizia, utume uliuchapa, Kwaheri, kwaheri, kwaheri Baba Padre.

2. (a) Sakramenti yaupatanisho, Baba ulitupatia

    (b) Mwili na Damu yake Yesu, Chakula cha roho zetu. Kwaheri, kwaheri, kwaheri Baba Padre.

3. (a) Ndoa za pamoja hakika, mawazo yako mazuri

    (b) Mwenyezi Mungu akulinde, Parokiani Vianzi. Kwaheri, kwaheri, kwaheri Baba Padre

4. (a) Vijibweni twakuombea, Maisha marefu Baba

    (b) Karibu tena Vijibweni, Nafasi uipatapo. Kwaheri, kwaheri, kwaheri Baba Lukumu.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa