Mtunzi: Eng.Richard Samson
> Mfahamu Zaidi Eng.Richard Samson
> Tazama Nyimbo nyingine za Eng.Richard Samson
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Zaburi
Umepakiwa na: Richard Samson
Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 2
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 29 Mwaka A
Mpeni Bwana utukufu na nguvu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu x2.
1. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, mwimbieni Bwana, nchi yote.
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, na watu wote habari za maajabu yake.
2. Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana, na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
Maana miungu yote ya watu si kitu, lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.
3. Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, mpeni Bwana utukufu na nguvu.
Mpeni Bwana utukufu wa jina lake, leteni sadaka mkaziingie nyua zake.
4. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu, tetemekeni mbele zake, nchi yote.
Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki, atawahukumu watu kwa adili.