Mtunzi: F. E. Nyanza
> Tazama Nyimbo nyingine za F. E. Nyanza
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Niwagira
Umepakuliwa mara 62 | Umetazamwa mara 56
Download Nota Download MidiTUTENGENEZE
EDENI MPYA (By F.Nyanza)
Dunia ilikuwa ni nzuri sana ilipotoka mikononi mwa Muumba,
nchi ilikuwa yenye kijani kibichi, maua mazuri misitu, mimea ya kila aina na
mito iliyo bubujika maji iliyo pamba dunia. Lakini kwa matokeo ya dhambi na
kiburi cha mwanadamu, ameiharibu dunia na uzuri wake umetoweka.
Dunia
imekuwa sikitiko
si
mahali pazuri pa mimea,
mimea
nayo mito ya asili
vingi
vimetoweka
Dunia si rafiki tena kwa kizazi cha mwanadamu amejitengenezea
kifo chake na kuiharibu hatima aliyo tengenezewa na Mungu.
Amekata
miti,
kachoma
misitu
kwa
shughuli zake
za
kila siku
ameyaharibu
mazingira;
Iko
wapi ile bustani ya Edeni ya kuvutia?
Iko
wapi ile Dunia ambayo Mungu aliserma;
Tazama
kila kitu ni chema (Ni chema) baada ya uumbaji wake.
Shime tuitengenezeni Edeni na kuurudisha uzuri wa
dunia. Tuipande miti na kuvutia viumbe na tuwarithishe watoto urithi ulio
mzuri. Pamoja tumpe Mungu utukufu na sifa kwa kazi yake.
Basi na
tusiiruhusu dunia iomboleze kutowajibika kwetu. Tutapata mvua, tukitunza
mazingira tutayaepuka magonjwa na pia tutauepuka ukame na joto kali hakika
vitatoweka duniani.
Tutengeneze Edeni mpya yawezekana kufanya hivyo, jukumu langu mimi na wewe.