Mtunzi: Joseph Mgallah
> Mfahamu Zaidi Joseph Mgallah
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Mgallah
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Joseph Mgallah
Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0
Download Nota Download MidiKIITIKIO
Tutawapa nini watu hawa x2 tazama (hapa ni nyikani nasi hatuna cha kuwalisha, tazama tunayo mikate mitano na samaki wawili, hata hivyo havitoshi kuwashibisha) x2
MASHAIRI
1. A. Yesu akachukua samaki na mikate akavibariki, akawapa wale, tazama wakashiba wote
B. Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano bila kuhesabu wanawake na watoto.
2. A. Nawe uonaye kiu na njaa sogea ulishwe, pia unywenshwe tazama atakushibisha
B. Neno la Mungu pia nia chakula cha uzima kinachotushibisha roho, tupokee tupate kushibishwa.