Ingia / Jisajili

Sadaka Hii

Mtunzi: Emanuel Chisunga Kasebe
> Mfahamu Zaidi Emanuel Chisunga Kasebe
> Tazama Nyimbo nyingine za Emanuel Chisunga Kasebe

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Emanuel Kasebe

Umepakuliwa mara 22 | Umetazamwa mara 32

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

SADAKA HII

Sadaka hii naitoa ni sadaka yangu ya leo (ni) nakuomba ipokee na uibariki Ee Bwana. X2

Ni sadaka ya Upatanisho (kati) yangu nawe Mungu wangu (ni) na kuomba ipokee na uibariki Ee Bwana. X2

1. Sadaka ninayotoa kwako ni sadaka ya ukweli, nimepata kwa juhudi za mikono yangu mitukufu (ni) nakuomba ipokee na uibariki Ee Bwana.

2. Ikupendeze Ee Bwana nimetoka kwa moyo wote, Sala zangu Dua zangu zipokee kila niombapao (ni) nakuomba ipokee na uibariki Ee Bwana.

3. Ni Pato langu la wiki nzima ninalileta mbele yako, Nia yangu na fedha zangu ninakutolea Mungu wangu (ni) nakuomba na ipokee na uibariki Ee Bwana.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa