Ingia / Jisajili

Kwa Maana Wewe U Mwema

Mtunzi: Vitus G. Tondelo
> Tazama Nyimbo nyingine za Vitus G. Tondelo

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Vitus Tondelo

Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 16 Mwaka A

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

Kwa maana wewe U mwema x2 Umekuwa tayari kusamehe x2

BETI

1. Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayaru kusamehe. Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao. Ee Bwana uyasikio maombi yangu; Uisikilize sauti ya dua zangu.

2. Mataifa yote uliowafanya watakuja; Watakusujudia wewe, Bwana. Watalitukuza jina lako; Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu. Wewe ndiwe mfanya miujiza, Ndiwe Mungu peke yako.

3. Lakini wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema. Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli, Unielekee na kunifadhili mimi.



Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa