Maneno ya wimbo
KIITIKIO
Ewe mwanadamu kumbuka umavumbi, na mavumbini utarudi.x2
MASHAIRI
-
Mwanadamu kumbuka kuwa umavumbi wewe na mavumbini siku moja utarudi.
-
Ulitoka katika tumbo bila ya mavazi na mavumbini siku moja utarudi.
-
Nasi pia inatupasa kukumbuka kuwa tutarudia mavumbini siku moja.
-
Mwanadamu ungama dhambi na ufanye toba na Mungu Baba atafuta dhambi zako.
-
Mwanadamu kumbuka kuwa una siku chache ulizopewa kuwa hai duniani.
-
Mwanadamu kumbuka kuwa u kama maua yachanuayo hatimaye hunyauka.
-
Na tumwombe Mungu Mwenyezi awahurumie awasamehe walioko Toharani.
-
Tumtukuze Mungu Baba pia Mungu Mwana tumtukuze naye Roho Mtakatifu.
-
Kama mwanzo sasa na siku zote na milele na milele na hata milele amina.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu