Mtunzi: Thomas J.Yotham
> Mfahamu Zaidi Thomas J.Yotham
> Tazama Nyimbo nyingine za Thomas J.Yotham
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Thomas Yotham
Umepakuliwa mara 7 | Umetazamwa mara 11
Download Nota Download MidiWIMBO WA JUBILEI
Kama mwali wa moto tumaini langu linawaka, wimbo wangu huu ukufikie: Chanzo cha uzima usio na mwisho, kwenye safari ya maisha nakutumainia.
Kila lugha, watu na Taifa, tunapata nuru katika Neno lako. Wana na Mabinti wanyonge waliotawanyika wanakusanywa kwa Mwanao mpendwa.
Ee Mungu, mpole na mvumilivu sana, ututazame sote: yazaliwe mapambazuko ya matumaini mapya. Mbingu na dunia zifanyike upya: pitisha ngome Roho wa uzima..
Inua macho yako, songa kwa upepo, kaza mwendo, Mungu anakuja, kwa wakati. Mtazame Mwana aliyefanyika mtu: maelfu kwa maelfu wanapata uzima.