Ingia / Jisajili

Ee Bwana Utuonyeshe

Mtunzi: Melchior Basil Syote
> Tazama Nyimbo nyingine za Melchior Basil Syote

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 5,748 | Umetazamwa mara 11,443

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ee Bwana utuonyeshe rehema zako (Ee Bwana) utupe wokovu wako x 2

  1. Na nisikie atakavyosema Mungu Bwana, maana atawaambia watu wake amani / hakika wokovu wake u karibu na wamchao, utukufu ukae katika nchi yetu.
     
  2. Fadhili na kweli zimekutana, haki na amani zimebusiana / kweli imechipuka katika nchi, haki imechungulia kutoka mbinguni.
     
  3. Naam, Bwana atatoa kilicho chema, na nchi yetu itatoa mazao yake / haki itakwenda mbele zake, nayo itazifanya hatua zake kuwa njia. 

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa