Ingia / Jisajili

Msakila Isaya

Mfahamu Msakila Isaya, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Mtwara Parokia ya Chihangu

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 508 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Mtwara

Parokia anayofanya utume: Chihangu

Namba ya simu: 0692277075 & 0764115205

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Isaya Katabwa Msakila ( Msakila Isaya ) ni mzaliwa wa Mpanda Mkoa wa Katavi, utume wake wa uimbaji umeanza mnamo mwaka 2006 akiwa miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaosoma music katika shule ya sekondari ya wavulana Songea ( Songea Boys' Sec School ) chini ya Mwalimu (Madam Mselewa ). Kuanzia mwaka 2007 alianza kuhudumu katika kwaya ya wanafunzi ( T.Y.C.S Songea Boys ), tangu hapo kipaji kiliendelea kukua na akaanza utunzi rasmi wa nyimbo. Baada ya kumaliza kidato cha nne 2009 aliweza kutumikia kwaya mbalimbali kwa kipindi kifupi zikiwemo, Kwaya ya Mt. Joseph, Kwaya ya Mt. Anton wa Padua ambazo zote hizo zinapatikana ndani ya parokia ya Usevya. Baadae alichaguliwa kujiunga na masomo ya A, LEVEL mwaka 2010 katika shule ya sekondari ya wavulana Kibiti ( Kibiti boys' Sec School ) ambapo aliendelea kuihudumia kwaya ya wanafunzi T.Y.C.S shuleni hapo huku akiitumikia kwaya ya Mt. Ludovick iliyo ndani ya parokia ya Kibiti wilayani Rufiji akihudumu nafasi ya mpiga kinanda hadi alipo maliza kidato cha sita mwaka 2012. Baada ya hapo aliitumikia kwaya ya Mt. Paulo kanisa la hija Sumbawanga kwa kipindi kifupi sana hatimae akachaguliwa kujiunga na masomo ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam mnamo mwaka 2012 October ambapo utume wake aliufanya ndani ya kwaya ya Mt.Philomena inayopatikana mabibo hostel-Ubungo mpaka alipohitimu masomo yake July 2015.

Hatimae alirudi nyumbani Sumbawanga na kupokelewa na kwaya ya Mt. Maria mama wa Mungu mnamo July 31st iliyo ndani ya kigango cha Knatalamba, Parokia ya Familia Takatifu-Kizwite ambayo anaitumikia mpaka sasa. Mpaka sasa kwa takribani miaka 11 ya utume wake amefanikiwa kutunga zaidi ya nyimbo 500 na baadhi ya nyimbo zikiweza kurekodiwa na kwaya mbalimbali.

Kufikia April 2017 Mwalimu Msakila aliajiriwa katika mkoa wa Mtwara wilaya ya newala ( Mwalimu Sec school) kwa masomo ya sayansi, na alijiunga na kwaya ya Mt. Fransico wa Asiz inayopatikana kigango cha mnyambe ndani ya parokia ya chihangu na ndipo anapoendeleza utume wake kwa sasa.

Mwl Msakila mpaka sasa ameshiriki katika uandaaji wa kazi/Albamu tatu ambazo ni:

* Tusali pamoja - Kwaya ya Mt. Philomena Mabibo hostel Dar es salaam mwaka 2013 ( Alishiriki kama Mwalimu )

* Paza Sauti - Kwaya ya Mt. Maria mama wa Mungu - Sumbawanga july 2016 ( Alishiriki kama Mwalimu na Mpiga kinanda katika albamuhiyo)

* Imani ya baba zetu - Mt. Martin - Mwanza december 2016

Mungu azidi kumlinda na kumbariki katika utume wake wa uimbaji ili aweze kusonga mbele zaidi Ameen.........