Ingia / Jisajili

Litukuzeni Jina La Mungu

Mtunzi: Fr. Gregory F. Kayeta
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Gregory F. Kayeta

Makundi Nyimbo: Anthem | Kristu Mfalme | Mafundisho / Tafakari | Shukrani

Umepakiwa na: Furaha Mbughi

Umepakuliwa mara 2 | Umetazamwa mara 5

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Litukuzeni, jina la Mungu daima milele, Enyi mataifa mshangilieni Mungu wenu. Kwakuwa Bwana ni mtukufu wa kutisha, yeye ni mfalme mkuu (wa dunia yote) msifuni Bwana kwa shangwe.

    [Jina la Mungu lihimidiwe daima milele, enyi mataifa lihimidini kwakuwa fadhili zake kwetu sisi zadumu daima milele] x2

1. Jina lake Bwana, litukuzwe sasa hata milele, Viumbe vya Bwana, msifuni Bwana Mungu wenu. Toka maawio hata machweo ya jua, Sifuni jina lake (Bwana Mungu wenu), Msifuni Bwana Mwenyezi.

Jina la Mungu...........

2. Enyi watumishi, msifuni Bwana kutoka mbinguni, mbingu nanyi maji, lisifuni jina la Bwana. Wafalme wa dunia nanyi watu wote, Wakuu nanyi wakazi (wote wa dunia), Msifuni Bwana Mwenyezi.

Jina la Mungu...........

3. Enyi Malaika, msifuni Bwana kutoka mbinguni, Jua mwezi nyota, msifuni Bwana wa mabwana. Majeshi yake yote na yamsifu Bwana, Yeye ndiye Mtawala (wa mabwana wote), Msifuni Bwana Mwenyezi.

Jina la Mungu...........


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa