Ingia / Jisajili

Thimotheus Mophath Sullusi

Mfahamu Thimotheus Mophath Sullusi, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Shinyanga Parokia ya Mater Misericordiae Cathedral- Ngokolo.

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 16 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Shinyanga

Parokia anayofanya utume: Mater Misericordiae Cathedral- Ngokolo.

Namba ya simu: +255766492729

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Historia yangu na uimbaji ilianzia siku tatu kabla kujiunga na darasa la Kwanza, ndipo nilipojiunga rasmi na uimbaji katika kwaya ya Mt.Maria, Parokia ya Murutunguru - Ukerewe.

Nilihitimu Shule ya msingi Mwenge (Shinyanga), St Pius X (Makoko seminary) kwa masomo ya Sekondari, Malangali Boys High school -Iringa na nilijiunga Jordan University College kwa elimu ya juu.

Ni mwalimu katika kwaya, mtunzi, pia nacheza kinanda kwa cha kawaida tu.

Ni muumini katika kujifunza sana Muziki kwaundani ili niweze kuelewa na kuutumia vyema katika kumtukuza Mungu wetu.

Katika majiundo ya  kimuziki nilianza kujifunza nikiwa Pre-Form one ambapo mwalimu wangu wa kwanza alikua hayati Mwl. I.P. Nganga kwa muda mfupi sana na badae nikiwa kidato cha kwanza sitawasahau wafuatao kwa mchango wao.

                                   i. Abel Jipili ambaye kwa sasa ni Frt.

                                   ii.Peter Respicius Magala

BAADA ya  masomo ya Sekondari nilikutana na E.F. Kidaluso, E.M. Ogeda, I.Nturama, DACHA Theonas, L. Cheyo, F.E. NYANZA ambao walinisaidia kwa nyakati tofauti. Hata hvyo uwepo wa MBJ. Mashamba tangu tukiwa masomoni ulisaidia ukuaji wa uelewa kwani tulishirikiana kwa karibu hasa katika kujifunza na kushirikishana vipaji ama uzoefu kwa yale tuliyopata kutoka kwa walimu mbalimbali.

Katika kucheza kinanda nilikuwa na walimu ambao walinisaidia kutoka zero ambao ni ERIC MALEZA akifuatiwa na Steven Luhende. Baada ya hapo nilikutana na walimu wengine wengi kwa nyakati tofauti wakanisaidia kuendelea kukua katika tasnia hii.

Watu ninaovutiwa nao katika tasnia ya Muziki wa kanisa ni wafuatao: INNOCENT MUSHI, HEKIMA MINDE RAYMOND, ERNESTUS OGEDA, F.E. NYANZA, B.D.WASONGA, V.MABULA.

Heshima kwa watunzi wa zamani itabaki palepale: MB SYOTE, JOHN MGANDU, JOSEPH MAKOYE, GF KAYETA, Fr. MALEMA, FAN na wengine wengi ambao wanazidi kunijenga pale ninapo kutana na nyimbo zao. Mchango wa ndugu hawa kwenye muziki wetu hautasahaulika.

Shukrani pia kwa Ftr. L. Temanya-OSA, Frt. B. Maro-CPPS, Br.Mwita-OFM-Cap na waseminari wote tulioshirikiana na kubadilishana uzoefu pamoja na walimu wote wa Kwaya ya Mt.Yohane Paulo II - Jordan University kwa vipindi tofautitofauti tulipokua hapo kimasomo. Ushirikiano ulikua mzuri na ulikuza vipaji vyetu wote. Bila kumsahau MBJ.Mashamba ambaye tumekua tukishirikiana kwa karibu tangu tulipokua wadogo hadi sasa tunaendelea kujifunza, kusaidiana,kupongezana na kukosoana kwa upendo mkubwa.

SHUKURUNI KWA KILA JAMBO, NI MAPENZI YA MUNGU KWENU. (1The. 5:18)