Ingia / Jisajili

Paul San. Mziba

Mfahamu Paul San. Mziba, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Mwanza Parokia ya Buswelu

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 12 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Mwanza

Parokia anayofanya utume: Buswelu

Namba ya simu: 0763661720

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

MWALIMU WA KWAYA, MTUNZI WA NYIMBO ZA DINI N.K, MPIGA KINANDA NA MWIMBAJI WA SAUTI YA NNE: Nimeanza utume wa uimbaji rasmi mwaka 2009 nikiwa kidato cha pili katika shule ya MOSHI TECHNICAL SECONDARY SCHOOL... katika kwaya ya Mtakatifu Sesilia hapo shuleni na kwaya ya shirika la Lejio Mariae hapohapo shuleni. Kujiendeleza kiutume wa uimbaji kuliimarika nikiwa kidato cha tano shule ya sekondari Usagara - Tanga katika kwaya yetu ya TYCS shuleni nikiwa kama mwalimu na mpiga kinanda; hali kadhalika wakati huo nilihudumu katika kwaya ya parokia ya Mtakatifu SLYVESTER- Parokia ya Mtakatifu M ATHIAS Mulumba - Usagara Tanga Hatimaye utume wangu uliendelea katika jimbo langu nililozaliwa- Mwanza katika parokia ya Buswelu katika kwaya Mtakatifu Thomas Mtume. Safari ya utume imeendelea mwaka 2014 -2017 nimehudumu katika kwaya ya Mtakatifu Gregory Mkuu - St. John's university of Tanzania. Pia kwaya mbalimbali ikiwemo kwaya ya Mtakatifu MARTINE de pores- chuo cha Afya Mirembe, kwaya ya Mwenyeheri Anuarite - St. John's university of Tanzania n.k Baada ya hapo niliendelea na utume katika kwaya mbalimbali Jimbo uuKatoliki la Arusha zikiwemo 1. Kwaya ya Mtakatifu PETRO- Parokia ya Mtakatifu M ATHIAS- Ngaramtoni 2. Kwaya ya Mtakatifu Gema Galgani- Parokia ya Kisongo 3. Kwaya ya kigango - Mukulati. Kwa sasa naendelea na utume wangu katika parokia ya Kiagata - Jimbo Katoliki la Musoma ambako ndio makazi yangu. NATUMIA MUDA MWINGI KUSOMA, KUANDIKA MUZIKI/NYIMBO KWA AJILI YA IBADA NA KAZI MBALIMBALI IKIWEMO MATAMASHA, NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU/RECORDING. PIA NATUMIA MUDA WANGU KUFUNDISHA KWAYA NA MUZIKI KWA WANAFUNZI WAHITAJI, PIA KUCHEZA VYOMBO VYA MUZIKI IKIWEMO KINANDA N.K. Pia kuandika nyimbo za watunzi mbalimbali kwa software mbalimbali na kuzipakia katika tivuti ya Swahili Music ili zipate kutumika na wengine kwa utukufu wa Mungu: Karibuni nyoote kwa huduma mbalimbali.