Ingia / Jisajili

Modest Tindegizile

Mfahamu Modest Tindegizile, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Bukoba Parokia ya Rukindo

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 37 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Bukoba

Parokia anayofanya utume: Rukindo

Namba ya simu: 0757431000

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Modest Tindegizile ni mwanakwaya, mtunzi na mwalimu wa uimbaji wa muziki wa Kanisa Katoliki. Nilianza kujifunza muziki 2003 nikiwa Drs la IV. Kipindi hiki nilifundishwa na Ndg. Novartus Tayebwa(alipata kujifunza muziki kupitia kanisa la Kiluther-under Germany sponsorship). Baadae nilijiunga na Seminary ndogo ya Mt. Don Boscombe Ruabon, ambapo nilijifunza kinanda na Muziki pia chini ya Fr. Novartis Rugoye ambaye kwasasa ni marehemu- Mungu ampumzishe kwa amani. Mwaka 2007 nilijiunga na Seminari ya Mt. Maria ya Rubya ambapo niliendelea kujiendeleza kimziki hasa kwa kufundisha na kucheza kinanda. Mpaka sasa nimeweza kutunga nyimbo sio chini 150 ambazo bado hazijawahi upload. Baadhi ya nyimbo cache zimerekodiwa. Mfano: Yesu alisema noon kwangu (Kwaya shirikisho USA River),Kama watoto wachanga (kwaya ya chuo cha ARUSHA University), Kama Ayala (Parokia ya Huruma Moshi), Sala yangu ipae ( Moshi), Msisumbukie maisha yenu (Kenya), Njoni enyi viumbe (Longido) n.k. Baadhi ya Parokia nilikowahi kuimba ni Parokia ya Rukindo, Kigango cha Ihunga-Rukindo, Parokia ya Korongoni Moshi, Parokia ya Msimbazi, Kwaya ya chuo kikuu cha Tumaini Makumira, Parokia ya Nzasa Temboni, Parokia ya Mt. Augustino Manundu Korogwe nk. Asante.