Ingia / Jisajili

John D. Gurty

Mfahamu John D. Gurty, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Mbulu Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Bashnet

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 107 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Mbulu

Parokia anayofanya utume: Moyo Mtakatifu wa Yesu Bashnet

Namba ya simu: 0693967117

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Utume wa Bwana udumu milele. TUMSIFU YESU KRISTO. Ndugu zangu kwanza nipende kutoa shukrani zangu Kwa Mwenyezi MUNGU anayetujalia Karama zote za Rohoni, pia kwa Waalimu wote wa Music Mt. Nawapenda sana: Kwa ufupi: nilizaliwa 31/8/1995 Katika Kijiji cha Long' kata ya Bashnet Wilaya ya Babati Mkoani Manyara. nilibatizwa nikiwa mtoto mchanga, Mama yangu ni Mkatoliki, na Baba pia Mungu Amlaze mahali pema peponi Amina. sikubahatika kusoma sana elimu. wakati ninaanza ujana niliacha sana kanisa, nilijaribu kuimba kwaya lakini ujana ulinizidi hata kwenda misa jumapili nikaacha, nilijikuta napenda sana mziki wa kidunia hasa bongo flava na nilijaribu pia kuuimba na nilikuwa na malengo nao, kumbe ndugu ni upotevu na uharibifu. Namshukuru Mungu kwa upendo wake kunifuata kule nilikotaka kupotelea nakumbuka siku yangu nilikuwa Arusha Nikakutana na mkono wa Mungu hakika sitasahau siku ile 21/ 11/2018 yalipo badilika Maisha yangu nikaacha hata kusikiliza music wa bongo flava jambo ambalo halingewezekana bila Mungu kwani ulikuwepo kila mahali hata migahawani. Lakini Mungu akaniambia unayaweza yote nikikutia nguvu. Niliokoka nikawa Mluthran lakini niliendelea kusali Mungu akasema wewe unapaswa kuwa Mkatoliki. Alijua yeye kwanini napaswa. Lakini baada ya kurudi katika Kanisa Katoliki nikakataa kurudi kuimba Kwaya Namshukuru sana Kaka yangu Martin Dominic alinilazimisha kurudi kuimba Kwaya ilikuwa mwaka 2019 mwanzoni baada ya kurudi kuimba Kwaya nikaipenda sana zaidi ya ule music wa bongo flava Kwaya ilikuwa tamu sana na tafakari zake, nikasema kwanini nisiwe Mwalimu wa Kwaya nikamtafuta Mwalim moja anaitwa Thomas. Mungu ambariki sana. Lakini baada ya mafanikio katika kujifunza Music bado kuna changamoto kubwa basi tunamshukuru MUNGU anatupigania kusonga mbele. Ndiyo history fupi ya mwanzo wa utume wangu Mungu anipe mwisho mwema. Asante sana. TUMWIMBIE BWANA KATIKA ROHO NA KWELI.