Ingia / Jisajili

CarlesJr

Mfahamu CarlesJr, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Tanga Parokia ya St. Mathis Mulumba Usagara

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 25 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Tanga

Parokia anayofanya utume: St. Mathis Mulumba Usagara

Namba ya simu: 0621-699596

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

CarlesJr. CarlesJr ni Jina la utunzi la Mwal. Wa Muziki anaejulikana kwa Jina halisi la Ubatizo kama Charles Sabas Luoga. Lililotokana na Jina la utani la baba yake huko kijijini kwao anaye itwa Mzee Kales nalo likabadilishwa uandikaji wake ukawa wa Kiingereza na kufanania Jina halisi la Mtunzi yaana Carles kama Charles. Hivyo mtunzi huyu hujiita CarlesJr ...Jr ikiwa inamaanisha Carles Mdogo. CarlesJr. Alizaliwa mnamo Tar. 12 Disemba 1994 huko Katika kijiji cha Ligumbiro Kata ya Mlangali Wilaya ya Ludewa Mkoa mpya wa Njombe. Alizaliwa na wazazi wake wawili.yaani. Sabas Charles Luoga baba yake na Relindis Jacob Mtitu mama yake. Wote wa kabila la wapangwa. Alianza masomo yake ya Muziki Rasmi alipo kuwa akisoma Pre Form one huko Matola Jimbo katoliki la Njombe ambapo alisoma kwa Mwaka mzima basic Music principles akiwa anafundishwa na Mwal. Matuye. Baadae aliendelea na mafunzo ya Muziki na Kinanda akiwa Seminari ya Awali ya Mt. Yosefu Kilocha huko Jimbo la Njombe. Hapo alipata nafasi za kushiriki kufundisha kwaya ya Shule na Kucheza kinanda mara chache. Baadae aliendelea kujifundisha zaidi kwa kusolve nyimbo mbali mbali mwenyewe. Baadae mwaka 2014 alipojiunga na Shule ya Upili ya juu ya Iyunga Tech huko Mbeya alikua akifundisha kwaya ya wanafunzi ambayo alikua ikifanya vzuri chini ya uongozi wake mpka kwenda kuimba Cathedral yaan Kanisa kuu la Jimbo huko Mbeya. Mwaka 2016 alipo hitimu alijiumga na Kwaya ya Mt. Sesilia Huko.Parokia ya Makambako Jimbo katoliki la Njombe aka endelea kujifua na kujifunza kinanda zaidi na nota zaidi. Mwaka 2017 alienda kujiunga na Chuo cha Afya na sayansi Shirikishi Tanga Wakati huo kikiitwa Chuo cha AMO na hivyo huko aliendelea kufundisha kwaya ya chuo na hapo chini ya uwalimu wake Kwaya hiyo ya Mt. Yusa thadei ilifanikiwa kuchukua Makombe mara tatu ya mashindano ya vyuo Kanda ya Tanga mjini. Baadae Alijiunga na Kwaya ya Mt. Silvesta Nankuendelea kufundisha kisha akajiunga na kwaya ya Mt. Yohane Parokia ya Donge huko.Tanga baadae akarudi tena Parokia ya Sahare na Kujiunga na kwaya kuu ya Mt. Mathias Mulumba. Huko aliendelea kufundisha na kutunga nyimbo mbalimbali. Naam hata sasa yuko anatumikia katika kwaya hizo mbili yaan kwaya ya Chuo cha Afya Tanga katika kwaya ya Mt. Yuda thadei na Kwaya ya Mt. Mathias Mulumba. Anapenda kuwashukuru wazazi wake kwa kumlea mpka kufikia hapo alipo Pia anawashukur Ndugu zake kwa kupambana kumsaidia kufikia malengo yake. Na anawashukuru wote wanao shirikiana nae Vizuri katika kulisongesha gurudumu la maisha yake pamoja na kifanya Utume wa kufundisha kwaya katoliki. Ujumbe. *MTUMIKIENI BWANA KWA FURAHA* Mungu akubariki wewe na Familia Yako AMINA.