Nimekuja Kuyafanya Mapenzi Yako

Mtunzi : John Mgandu

Category : Mwanzo | Zaburi |

Uploaded Na : Yudathadei Chitopela > Mfahamu zaidi

Weka wimbo kwenye favorites

Umetungwa Dar es Salaam, tarehe Aug 07, 1990

Umetazamwa mara 3,356

PDF imekuwa downloaded mara 1,321

Wafahamishe wengine juu ya wimbo

Ndipo niliposema, tazama nimekuja Bwana nimekuja, tazama nimekuja kuyafanya mapenzi yako x 2

  1. Nalimngoja Bwana kwa saburi, akaniinamia akakisikia kilio changu, akatia wimbo mpya kinywani mwangu ndiye sifa zake Mungu wetu.
     
  2. Dhabihu na matoleo hukupendezwa nayo, masikio yangu umeyazibua, kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka, ndipo niliposema tazama nimekuja.
     
  3. Katika gombo la chuo nimeandikiwa, kuyafanya mapenzi yako, mapenzi yako, ee Mungu wangu ndiyo furaha furaha yangu, naam sheria yako i moyoni mwangu.
     
  4. Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kusanyiko kubwa, sikuizuia midogo yangu, ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana unajua. 


Mtunzi huyu ana nyimbo 132 SMN

Maoni

Maoni 0