Nirudieni Mimi

Mtunzi : Aloyce Goden

Category : Juma Kuu | Kwaresma |

Uploaded Na : Vusile Silonda > Mfahamu zaidi

Weka wimbo kwenye favorites

Umetungwa Chang'ombe Dar es salaam, tarehe May 26, 2005

Umetazamwa mara 7,957

PDF imekuwa downloaded mara 2,125

Wafahamishe wengine juu ya wimbo

Kiitikio:

 

Lakini hata sasa asema Bwana nirudieni, mimi kwa mioyo yenu yote x 2

 

Mashairi:

1. Fanyeni mabadiliko mioyoni mwenu, kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza - nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote.

2. Pigeni Tarumbeta huko Sayuni, waambieni watu wote ili wafunge - nirudieni mimi...

3. Kusanyeni watu wote waleteni kwangu, waleteni na watoto hata wazee - nirudieni mimi ...

4. Mpingeni yule mwovu atawakimbia, nikaribieni nami nitawakaribia - nirudieni mimi ...

5. Takaseni mikono yenu iliyojaa dhambi, safisheni mioyo yenu yenye nia mbili - nirudieni mimi ...

 

 Mtunzi huyu ana nyimbo 6 SMN

Maoni

Maoni 2

benito adam

Aug 24,2016

Pongeza, Kosoa.... Uwe mstaarabu

thompson shuma

Jul 22,2016

wimbo mzuri unahiti vizuri hongera sana tunasubiri video kama inakuja