Nirudieni Mimi by Aloyce Goden

    Home > Kwaresma > Nirudieni Mimi    

Je unatafuta wimbo? > Request a song here


Je wimbo huu una makosa? Report This Song

Maneno ya Nirudieni Mimi.

Kiitikio:


Lakini hata sasa asema Bwana nirudieni, mimi kwa mioyo yenu yote x 2

 

Mashairi:

1. Fanyeni mabadiliko mioyoni mwenu, kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza - nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote.

2. Pigeni Tarumbeta huko Sayuni, waambieni watu wote ili wafunge - nirudieni mimi...

3. Kusanyeni watu wote waleteni kwangu, waleteni na watoto hata wazee - nirudieni mimi ...

4. Mpingeni yule mwovu atawakimbia, nikaribieni nami nitawakaribia - nirudieni mimi ...

5. Takaseni mikono yenu iliyojaa dhambi, safisheni mioyo yenu yenye nia mbili - nirudieni mimi ...

 

Nota za Nirudieni Mimi


Mtunzi: Aloyce Goden

Umetungwa: 26-05-2005

Mahali: Chang'ombe Dar es salaam

Categories: Kwaresma, Juma Kuu

Uploaded by Vusile Silonda

Weka kwenye My Favorites

MIDI ni sauti (mlio wa wimbo). Ili ku-download midi, Right Click > Download Midi Kisha Chagua "Save Link As" or "Save Target As".
Nota za Nirudieni Mimi