Asilegee Moyowe by John Mgandu

    Home > Kwaresma > Asilegee Moyowe    

Je unatafuta wimbo? > Request a song here


Je wimbo huu una makosa? Report This Song

Maneno ya Asilegee Moyowe.

1.       Asilegee moyowe asitoke machozi machozi akimkumbuka Munguwe kwa yake makombozi mtoa roho msalabani mtaka kufa mwenyewe kwasababu kumpendani na ni mfunga moyowe?

2.       Bustani mle Getsemani amwomba Mungu Baba Mungu Baba Je! Mtu Mungu ana nini nguvu zake ni haba. Rabbi yangu waziona dhambi za binadamu binadamu Mwili wake umetona kama jasho la damu

3.       “Salamu Rabbi Salamu” anena Yuda mbaya Yuda mbaya Mwenye moyo wake mgumu ambusu pasi haya aliwaambia basi “Ntakaye mbusu ndiye mtwaeni na kwa upesi” Yuda nani? Nisiye

4.       Yuda nani? Ila yeye aliyetenda dhambi tenda dhambi akikosa kwa Mungu we mtenda kwa hia na dhambi mwenye kumtendea mema mtaka dhambi haoni kwamba ni kutupa neema kumwendea shetani

5.       Wote ni kupiga mbio mitumewe pamoja pamoja wamtia mikono yao askari walokuja wampeleka hukumuni aamuliwe na mtu mwenye kutoka uwinguni mkuu wa watu

6.       Mtume Petro amkanusha amenena “simjui” “simjui” Uhodari umekwisha machoye hainui Pilati amwona Rabbi hakukosa ‘ta neno hata neno asema “sioni dhambi” lakini ni mwoga mno

7.       Hauthubutu kumwachia si hukumu aomba aomba mmoja nitamfungulia Yesu au Baraba. Wayahudi mwamtakani Baraba aachwe tu aachwe tu Yesu afe msalabani damuye juu yetu

8.       Pilati hukumu gani “Simo nanawa mkono mkimtaka Yesu mwueni” La mwamzi hilo neno? Mara askari wamwaza nikupiga kelele kelele kumcheka na kumchokoza mwenye mema milele

 

 

 

 

Nota za Asilegee Moyowe


Mtunzi: John Mgandu

Categories: Kwaresma

Uploaded by Lawrence Nyansago

Weka kwenye My Favorites

MIDI ni sauti (mlio wa wimbo). Ili ku-download midi, Right Click > Download Midi Kisha Chagua "Save Link As" or "Save Target As".
Nota za Asilegee Moyowe