Michango kwa ajili ya Swahili Music Notes kwa mwaka 2018

Gharama kwenye kutuma nyimbo za Jumapili:
Ni jambo la kumshukuru Mungu kuona kuwa website yetu inakuwa, na inaendelea kuwafikia watu wengi kwa ajili ya kuwasaidia kupata nyimbo za vipindi mbalimbali vya kanisa. Kudhihirisha hilo, idadi ya watu wanaopokea email za nyimbo za kila Jumapili imefikia 2006. 

Lakini pamoja na kukuwa huku, basi kuna gharama ambazo zimeanza kuhitajika. Huduma (Service / System) ninayoitumia kwa kutuma hizi emails inaitwa Mailchimp (Unaweza kuifahamu zaidi kwa kubofya hapa > http://mailchimp.com/), ni huduma ya kimataifa kwa ajili ya kutuma emails nyingi kwa wakati mmoja (Mass emailing, email marketing). Niliichagua maana inarahisisha kazi sana, na inanipa ripoti za kutosha juu ya upokeaji wa email za nyimbo. Huduma hii, hutolewa na mail chimp bure kwa orodha yenye watu wasiozidi 2,000. Wanapozidi 2,000, basi kuna gharama ambayo Mail Chimp inachaji. Kwa sasa gharama hizo ni $30 (Dola za kimarekani thelathini, ambazo ni sawa na ~66,000 za Kitanzania) kwa mwezi. Hivyo akaunti Swahili Music Notes italazimika kulipia ~66,000 kila mwezi kwa ajili ya kuendeleza huduma hii. [ieleweke, SIO 66,000 kwa kila mtu, ni akaunti].  Bado najaribu kuwaomba wahusika punguzo au kuondolewa kwa gharama, ila mpaka sasa sijafanikiwa.

Ombi kuu hapa, ni kuomba wenye mapenzi mema, wachangie ili kusaidia kupunguza gharama hizi. Naomba ieleweke kuwa, hii haimaanishi kuwa unapaswa kulipia ili upate email za nyimbo, la hasha. Hili ni ombi tu kwa wale watakaoweza, na watakaopenda kuchangia. Michango yaweza kutumwa kupitia namba 0715556327 au 0768 205 729 (Jina Vusile Silonda). Na michango yote itaonekana kwenye ukurasa huu.

Mapato: yatakuwa rangi hii

Matumizi: yatakuwa rangi hii

Date Details Income (Tshs.) Expenditure (Tshs.)
01-01-2018 Salio kutoka mwaka 2017 2,854,821
22-02-2018 JUMLA 2,854,821 0

Salio ni 2,854,821

Kuchangia: +255 715 556 327 (Tigo Pesa), +255 768 205 729 (M-Pesa).