The New Directory

Ninafurahi sana ninapopata changamoto kutoka kwa baadhi ya watumizi wa Website ya Swahili Music Notes. Mawazo yao huwa yananifanya niongeze juhudi zaidi katika kuboresha chombo hichi.

Changamoto ya hivi karibuni imetoka kwa Mratibu wa Kapotive Singers, Ndugu Andrew Kagya. Yeye alipendekeza tuwe na Directory ya Watunzi wa nyimbo. Wazo hili nililishalifanyia kazi, kwa kiasi fulani, lakini kwa kweli lilikuwa bado halijakamilika. Na kwa kweli, nilikuwa bado sijapata njia nzuri ya kulimalizia hili wazo mpaka ndugu Andrew alivyonishirikisha wazo lake.

Directory mpya ambayo utaipata hapa kwa kubofya hapa, ina vitu vikuu vitatu. 

  1. Watunzi.
  2. Shule za Muziki.
  3. Studio za kurekodi. 

Mpaka sasa hatuna shule za Muziki wala Studio, ila nina imani zitapatikana tu.

Directory hii ina nafasi kubwa sana ya kukua. Kama una wazo la kundi lingine lolote linaloweza kufit hapa kwenye directory, nitaarifu. 

Huu ni mfano wa hilo > http://www.swahilimusicnotes.com/piano/composer/terence-vusile-silonda