Ingia / Jisajili

Namna ya Ku-Upload na Ku-Edit Nyimbo kwenye Swahili Music Notes

Watu wengi wanapenda kuchangia Swahili Music Notes kwa ku-upload nyimbo. Muongozo huu ni kuwasaidia wale ambao hawajaweza ku-upload nyimbo bado:

 

  • Kwanza kabisa, kabla ya ku-upload nyimbo, ni vyema kuzichora vizuri kwa kutumia software mbalimbali za kuchorea nyimbo ambazo zipo. Kuna Capella, Kuna Muse Score. Uchoraji mzuri, wa usafi na wa kuzingatia kanuni za muziki, ndio utaharakisha nyimbo kuwa reviewed pale utakapo-upload.
  • Pili, ukitaka ku-upload nyimbo, ni lazima uwe mtumiaji uliyesajiliwa (registered) wa Swahili Music Notes. Waweza ku-register hapa > http://www.swahilimusicnotes.com/auth/register
  • Baada ya kuregister, utalazimika ku-confirm account yako, kwa kwenda kwenye email yako na kufuata maelezo ya email yaliyotoka Swahili Music Notes. Kama haipo kwenye inbox, basi cheki kwenye Spam. Kama imechelewa, basi mtaarifu Admin.
  • Baada ya ku-confirm account yako, utaweza ku-login kwa kupitia links zilizo upande wa juu kulia. 
  • Baada ya ku-login, upande wa juu kulia, utaona link imeandikwa Dashboard. Click kwenye hiyo link.
  • Kama ni mara yako ya kwanza, itakulazimu kwanza ukubaliane na mwongozo kabla ya kuanza ku-upload.
  • Ukishakubaliana na mwongozo, utaona link za ku-upload nyimbo ambazo zitakuwa juu kushoto.
  • Tafadhali tumia fomu iliyo kwenye Contact Us page kuuliza swali kama hujaelewa

 

Je ni namna gani ninaweza ku-edit wimbo baada ya ku-upload?

  • Kuna sababu kadhaa za kuedit wimbo baada ya ku-upload kama:
    • Baada ya ku-upload, admin alikutaarifu (Kabla ya ku-review), kuwa kuna makosa ya kurekebisha.
    • Baada ya kuwa-reviewed, nota zilizochorwa vizuri zaidi, au umependa kuboresha wimbo n.k.

 

  • Ili ku-edit, KABLA WIMBO HAUJAWA REVIEWED. Nenda kwenye Songs Pending Review, kisha bonyeza Alama ya Penseli iliyo kulia kabisa ya wimbo unaotaka ku-edit. Nenda kwenye sehemu ya PDF, delete hiyo PDF  (na midi), kisha upload mafile ambayo umesharekebisha.

 

  • Ili ku-edit, KABLA WIMBO USHAKUWA REVIEWED. Nenda kwenye Approved Songs, kisha bonyeza Alama ya Penseli iliyo kulia kabisa ya wimbo unaotaka ku-edit. Nenda kwenye sehemu ya PDF, delete hiyo PDF  (na midi), kisha upload mafile ambayo umesharekebisha.

 

  • Unapo edit wimbo, mabadiliko ufanyika mara moja.

  • MUHIMU: Unaweza ku-edit wimbo ulio-upload wewe tu. Hata kama wimbo umetunga wewe, lakini umekuwa-uploaded na mtu mwingine, hautaweza ku-edit. Tafadhali wasiliana na admin ili akusaidie.