Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je, nitapataje email za nyimbo za Mwanzo na Katikati pamoja na nyimbo zilizokuwa uploaded karibuni?

 

 • Ni rahisi. Unahitaji ku-register kwa kwenda kwenye ukurasa huu > http://www.swahilimusicnotes.com/register
 • Baada ya ku-register, italazimika uende kwenye email inbox yako, ili kuhakikisha kuwa email uliyoiweka kwenye website ni sahihi. Utakuta email kutoka kwa Swahili Music Notes. Fuata maelekezo ya kwenye hiyo email.
 • Baada ya hapo, utaanza kupokea email za nyimbo mbalimbali.
 • Tafadhali tumia fomu iliyo kwenye Contact Us page kuuliza swali kama hujaelewa

Mimi napenda sana ku-upload nyimbo, lakini sijui nifanyeje ili niweze ku-upload. Je, kuna utaratibu gani?

 

 • Ukitaka ku-upload nyimbo, ni lazima uwe mtumiaji uliyesajiliwa (registered) wa Swahili Music Notes. Waweza ku-register hapa > http://www.swahilimusicnotes.com/register
 • Baada ya kuregister, utalazimika ku-confirm account yako, kwa kwenda kwenye email yako na kufuata maelezo ya email yaliyotoka Swahili Music Notes. Kama haipo kwenye inbox, basi cheki kwenye Spam. Kama imechelewa, basi mtaarifu Admin.
 • Baada ya ku-confirm account yako, utaweza ku-login kwa kupitia links zilizo upande wa juu kulia. 
 • Baada ya ku-login, upande wa juu kulia, utaona link imeandikwa Dashboard. Click kwenye hiyo link.
 • Kama ni mara yako ya kwanza, itakulazimu kwanza ukubaliane na mwongozo kabla ya kuanza ku-upload.
 • Ukishakubaliana na mwongozo, utaona link za ku-upload nyimbo.
 • Tafadhali tumia fomu iliyo kwenye Contact Us page kuuliza swali kama hujaelewa

Mimi ni mtunzi, ila siwezi kubadili taarifa zangu zilizomo kwenye site.

 • Kama umesharegister, basi mtaarifu admin.
 • Kama bado hauja-register, basi register kisha mtaarifu admin naye atakusaidia uweze kubadili taarifa zako.
 • Tafadhali tumia fomu iliyo kwenye Contact Us page kuuliza swali kama hujaelewa

Mimi nafurahia huduma inayotolewa na Website hii. Ningependa kuchangia, je nifanyeje?

 

Kuna njia nyingi za kuchangia Swahili Music Notes:

 

 • Kwanza kabisa, wataarifu wengine wasioijua Swahili Music Notes. Kwa kufanya hivi utasaidia kufikisha nyimbo kwa wahitaji wengi zaidi.
 • Pili, waweza ku-upload au ku-scan na kutuma kwa admin nyimbo mbalimbali, hasa zile ambazo zinaombwa na wengine.
 • Tatu, waweza kujitolea kufundisha vitu mbalimbali, mfano muziki kwa njia ya maneno (maelezo) yatakayokuwa kwenye website hii (Bado linafanyiwa kazi).
 • Nne, waweza kujitolea kukagua nyimbo. Pia waweza kujitolea kuchapa lyrics za nyimbo ambazo hazina maneno.
 • Tano, waweza kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za Website kama ilivyoelezwa kwenye ukurasa huu > http://www.swahilimusicnotes.com/donations
 • Tafadhali tumia fomu iliyo kwenye Contact Us page kuuliza swali kama hujaelewa

Mimi napenda kujifunza muziki, je unaweza kunisaidia?

 

Ondoa shaka, Swahili Music Notes ina lengo la kuwakutanisha walimu na wanafunzi wa muziki. Tafadhaili bofya link inayofuata ili uone shule mbalimbali za muziki zilizoweka taarifa zake kwenye Swahili Music Notes.

http://www.swahilimusicnotes.com/directory

Je, shule / studio yangu / kundi langu laweza kuweka taarifa yake?

 

Ndio inawezekana, tafadhali wasiliana na Admin kwa kupitia form kwenye Contact Us